ILI UWEZE KUFANIKIWA IJUE SIRI HII

MOJA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA LAZIMA UJIFUNZE KUWA MVUMILIVU

  Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara inakupasa kuwa na uvumilivu huwezi anza biashara leo na ufanikiwa leo leo itachukuwa muda na inategemea na aina ya biashara unayofanya
      Hapa nakueleza kitu cha msingi sana na kitakusaidia sana katika kufanya biashara yako Lazima ukubali kuwa mvumilivu. Inawezekana ikatokea mapema Zaidi ya miaka mitano kutokana na aina ya kile unachokifanya. Pia inawezekana ukapata nguvu kubwa kutoka kwa watu ambao watakuja kukusaidia ukavuka haraka lakini mimi sikufundishi juu ya vitu ambavyo havitokani na nguvu yako mwenyewe. Ni kweli unaweza kufanikiwa kufikia hao elfu moja mapema Zaidi kulingana na watu ambao ulionao wewe. Na inaweza kuchukua hata miaka 5 hadi kumi kwa mtu kuweza kufikia kwenye elfu moja.

Unajua watu elfu moja wanaweza kukupa kitu gani? Tusema hao watu elfu moja wanaweza kununua bidhaa kwako ambazo kwa jumla ndani ya mwezi mmoja utaweza kutengeneza tsh elfu kumi tu kwa kila mmoja yaani kama shilingi mia tatu tu kwa siku. Ukizidisha 1000×10,000 kwa mwezi utaweza kutengeneza shilingi milioni kumi.

Hiyo elfu kumi ni mahesabu madogo sana lakini unaweza kuwa na vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kukupa faida kubwa Zaidi. Kumbuka hao watu elfu moja wkaishakuamini unaweza kutengeneza bidhaa yeyote mpya na ikanunuliwa kwa haraka sana kwasababu walishakuamini tangu zamani.

Cha muhimu wewe ni kuendelea kufanyia kazi kile ambacho unakifanya. Weka malengo makubwa ambayo yatakusukuma kila siku uchukue Hatua. Fanya kazi kwa bidi. Hakikisha hakuna mtu mwingine anaweza kukuta yaani tumia ule uwezo wako wa kipekee kwenye kile unachokifanya.

Ili uweze kuwafikia hao watu elfu moja hutakiwi kuishia Njiani. Usikatee tamaaa fanya kazi kwa bidii ,tangaza biashara yako hata wakati mwingine kwa kutoa ofa kwa wateja wako ,tengeneza wateja endelevu na utaona mafanikio na utaona mabadiliko na utakuwa kibiashara

  Asante sana endelea kunifuatilia kwenye makala zangu uendelee kupata elimu ya kukuvusha upige hatua kufikia mafanikio yako

  Kwa mawasiliano au ushaur zaidi
  Whatsup namba +25573637565

Comments

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE