JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE

UNGA WA LISHE.


             Unga lishe ni unga kwaajili ya chakula ulio na
mchanganyiko wa viini lishe vyote muhimu. Mara
nyingi unga huu hutumiwa kuandalia uji. Wakati
mwingine utengenezaji wa unga huu huzingatia
walengwa walio kusudiwa kuutumia.Hii ni ili kuweka
viini lishe vinavyo endana na mtumiaji. Pia unaweza kutengeneza unga lishe kwa matumizi
ya jumla ambao unafaa kutumiwa na mtu yeyote.
Unga huo uwe na mchanganyiko wa nafaka zifuatazo:


*KANUNI ZA KUANDAA UNGA WA LISHE.*

Vifaa
=ulezi kg 1
=mahindi yasiyokobolewa kg 1/2
=ngano isiyokobolewa kg 1/2
=karanga kavu ila mbichi 1/2
=soya isiyobanguliwa 1/2.

*Njia ya kuandaa.*

1) chukua ulezi wako upete vizuri kwenye ungo.
Kisha weka kwenye maji kuupembua. Hakiksha
kwamba unaupembua mara nyingi zaidi kwa kutumia
maji masafi na chombo cha bati hadi mawe/
mchanga uishe wote kabisa. Kumbuka kwamba
ulezi huwa michanga sana.
hivyo matumizi ya vitu vya bati au chuma wakati wa
kupembua hukufanya uweze kuona mawe vyema,
pia mawe yasiteleze sana as yanakuwa kama
yananatiana na chuma hivi. Hivyo muda wa kupembua
kuwa mchache tofauti na ukitumia chombo cha
plastic.

2)Ukishahakikisha ulezi wako ni msafi basi tenga
ungo wako kisha umimine ulezi na uanike juani ili
ukauke kabisa.

3) Peta mahindi yako vyema toa yote yaliyo mabovu,
peta ngano yako toa punje zote zilizo mbovu kisha
osha vizuri kwa maji ya kutosha na anika kwenye
ungo wake tofauti.

4) Peta na chagua soya, kisha chemsha soya zako
jikoni kwa dakika 10 zitokote, kisha anza kuzimenya
maganda, ni rahisi as yanakuwa yanamenyeka kwa
kuteleza hivyo ukifikicha mkononi tu yanatoka.
baada ya kutoa maganda yote anika hizi soya
kwenye ungo wake hakikisha zinapigwa jua sana zikauke kabisa ziwe kama vile hazijagusa maji
kabisa.

5) Zikisha kauka kabisa zitie kwenye sufuria na
moto mdogo sana anza kuziaanga kama vile
unakaanga karanga ama ziweke kwenye oven *60 degree* kwa nusu saa. Zikitoka kwenye moto ziweke
sehemu ya wazi ili zipoe bila kupeana unyevu.

6) Chagua karanga zako vizuri, hakikisha kila punje
mbovu unaitoa (jamani naomba niseme wazi kila
karanga mbovu itolewe) kisha zikaange kwa moto
mdogo sana ziwe kavu kabisa lakini zisiungue ama
ziweke kwenye oven kwa 60 degree for 15-20 mints.
ukishazikaanga zianike tena juani ili zipoe lakini zipoe
bila kuabsorb moisture kabisa.
zikishakauka kabisa zidunde kama mbegu ya ubuyu
basi zimenye maganda yote kisha upete halafu
uchague zile punje nzuri tu ambazo hazina rangi ya
njano ama hazina kutu.

7) Hakikisha nafaka zako hizi zimekauka
sana na hakuna hata punje moja mbovu ndipo
uziweke pamoja na kuazisaga mashineni. Hakikaisha
pia unga unaposagwa unarudiwa mara ya pili ili uwe
mlaini usiwe na chenga chenga.

8) Baada ya kusaga anika unga wako mahali pakavu
hadi upoe, na hakikaisha wakati wa kuanika
hautachafua. Kuwa salama zaidi ni bora ukajitahidi
nyumbani ukawa na kitambaa ambacho unakiweka
juu ya ungo wako kisha unamimina unga wako,
ukiuweka juani tafuta kitambaa kingine kilicho cha
nyavu nyavu uweke kwa juu kufunika unga wako
usifuatwe na wadudu ama kupata uchafu.
Ukisha kauka tafuta chombo kikavu uweke na
ufunike vizuri kisiwe na sehemu ya kupitisha
wadudu.

Hifadhi unga vizuri kwa ajili ya matumizi au weka kwenye vifungashio tayari kwa biashara.

Comments

  1. Ubarikiwe sana nataka kuanza kufanya hii biashara nilikuwa sijui nianzie wapi ,,ubarikiwee Sana aiseee

    ReplyDelete
  2. Me nataka nitengeneze kama ulivyo elekeza ivyo lakini nataka nifungashe vzr ,kifungashio kiwe labeled vzr ..je nifwate taratibu zipii??

    ReplyDelete
  3. Naomba msaada nianzie wapi? Ili nifungashe vzr unga wangu?..

    ReplyDelete
  4. Mi naona una tudanganya kabisa, unga wa lishe unatakiwa kuzingatia makundi matango ya chakula, hapo umesema (ulezi, mahindi, ngano, zote ni wanga) kwanini kurudia rudia wanga?

    ReplyDelete
  5. Tusaidie bas Joyce wetu. Na sisi tuelewe make wengine hatujui ndo maana tupo hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna makundi matano ya Chakula
      1. Nafaka, vyakula vya mizizi na ndizi mbichi ( mahindi, ulezi,mchele, ngano, mtama, mihogo,magimbi, viazi nk)
      2. Vyakula vyenye adili ya wanyama na mikunde ( Maziwa, mayai, nyama, samaki, kumbikumbi nk)
      3. Mbogamboga ( mboga za majani
      4. Matunda
      5. Mafuta na sukari
      Hayo ndio makundi muhimu ya vyakula kama hujapata yote bado hujakamilisha lishe

      Delete
  6. Me naona hajakosea kwasababu makundi ni wanga na protein tayar kuna karanga na soya, tena huu ni mchanganyiko mzuri unaweza tumiwa na watu wa rika zote hata wenye upungufu wa kinga. Au ulitaka aweke mbegu za maboga mbegu za mchicha ambazo ni protein pia. Hata angeweza kupunguza wanga moja iwe michanganyo minne yani wanga 2 na protein 2 ni sawa. Lakini huzidishwa wanga kwasababu watoto wanaitaji wanga zaidi kukua. Na kumbuka hata anaeweka wanga pekee ana maana yake pia. Ni vizuri kubadilisha mara kwa mara izi nafaka kwa ajili ya lishe ya mtoto, sio kumpa mtoto nafaka zile zile January to December.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtoto anahitaji protein zaidi tena hasa ya kutoka KWA wanyama! Maziwa,mayai, nyama na samaki! For sure ukimpa mtoto wako huo uko na ukakosa hivyo vitu utapiamlo unamwita

      Delete
  7. Amesema kwa mtu yeyote je kwa yule mwenye tatizo la kisukari imekaaje,maana kweli mchangayo huo unaonekana una kiasi kikubwa cha wanga kuliko protin

    ReplyDelete
  8. Mmmmmmhhh! Unamaelezo mazuri sana lakini hujakua specific huo kwa mtoto mdogo 6 months haumfai Kwani hataweza kuumeng'enya pia una vitu vingi kama ana aleji hutagundua ni kipi kimemkataa. Over all hatushauri kusaga karanga pamoja but karanga iandaliwe peke yake na iwekwe wakati wa kupika kama kwenye mboga. Kwani huvuta unyevu na kutengeneza sumukuvu! Lakini pia mahindi, michelle, ngano na ulezi ni vyakula vya kundi moja so anya of them inatosha

    ReplyDelete
  9. Wapendwa nauza unaga walishe kilo moja 4000. Kama pia natengeneza lishe kwamteja anaye taka kutengenezewa kwa jumla

    ReplyDelete
  10. Nahitaji kujua unapatkana mkoa gani na wilaya ipi

    ReplyDelete
  11. Lishe nzuri kwa mtt inatakiwa isizidi aina 3 za machanganyiko, pia karanga sio salama kuchanganya wakat wa maandalizi ya unga.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI