JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUFULIA

Sabuni ya maji kufulia

Mahitaji

Salifoniki acid kilo 1

Sodash robo kilo
Maji lita 20
Slesi robo kilo
C.D.E vijiko vitano vya chakula


Gricelini vijiko 15 vya chakula

Chumvi ya viwandan kilo 1

C.M.C vijiko vitano vya chakula

Pafumu kijiko 1 cha chakula

Rangi kijiko 1 chai

    Hatua

Andaa ndoo ya plastik kisha weka salifonic acid,ikifuatiwa na sodash iliyochanganywa na maji na uanze kukoroga,weka maji na ukoroge mpaka vichanganyikane vizur

2)wakati ukiendelea kukoroga weka sles,c.d.e na gricelin na uendelelee kukoroga

3)Tia chumvi na uikoroge mpaka ilainike vixuri kisha weka c.m.c kidogo kidogo kwa kunyunyuzia huku ukiendelelea kukoroga,kisha weka rangi na perfumu na uendelelee kukoroga kwa dakika 10-15

4)Baada ya hapo iache kwa saa 24 na itakuwa tayar kwa matumiz

NB:Kazi za malighafi
C.d.e kulaininisha maji

Gricelin kulainisha nguo

Chumvi kutia uzito

C.m.c kuongeza uzito jinsi unavyotaka

Comments

  1. Tafadhali mwalimu naomba ufafanuzi wa herufi hizi C.D.E na C.M.C namba ya Wassap 0622193534

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE