JIFUNZE NIDHAMU YA PESA

MAMBO MATANO YATAKAYOKUSAIDIA KUWA NA NIDHAMU JUU YA PESA

   Fuatana nami twende tukajifunze maana hili eneo ni changamoto kwa walio wengi  wetu na ndipo makosa makubwa yanapofanyika na tunaishia kulalamika tyuu
 
        Mambo muhimu na ya msingi kabisa

1)Kubali tatizo ulilonalo kuwa ni lako mwenyenyewe,kiri tatizizo la kutokuwa na matumizi sahihi ya mara tuu upatapo pesa  ,halafu tafuta suluhisho la tatizo lako ufanye nini cha kukuwezesha kuachana na matumizi mabovu ya pesa

2)Jifunze kuweka malengo ya maisha au kile ambacho unakifanya kifanikiwe na uwe na nidhamu nacho na kikifanya kiwe cha kwanza kwako kuliko mambo mengine na ukipata pesa peleka kwenye malengo makubwa kwanza,mfano umejiwekea malengo baada miez mitano unataka ujenge nyumba,au nifungue biashara  nk hakikisha unapopata pesa ipeleke kwenye ujenz,au biashara uliyokusudia kwanza

  3)Kuwa na mpango mkakati( plani)Hata kama hauna pesa kwa muda huo jiweke mkakati au mbinu bora kwa kuweka akiba ya pesa ili uweze kufikia malengo uliyojiwekea

4)Taarifa za mpango mkakati wako( mapitio ya kaz yako umefanya vizuri wapi,umekosea wapi ili urekebishe hilo eneo na kuboresha zaidi ili makosa yasijirudie tena

5)Standard life yako) Hii ndio sehemu muhimu kabisa  ,ni lazima ujue kupanga matumizi  yako vizuri,na mara nyingi kabla mtu hajapata pesa huwa anapanga mipango mingi sana laki akishapata mipango yote hupotea na kuanza matumiz mengine yasiyo na umuhimu ikiwa kununua vitu ambavyo hajapanga kununua mwisho wa cku anajikuta pesa imekwisha na kuishia kulalamika bila kutimiza malengo yake ,kitu kingine ni kuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako ,unapata kidogo ,matumizi yako juu hii ni hatari sana hivyo ni muhimu sana kupanga matumizi yako au bajeti vizuri ukizingatia haya utaweza kusonga mbele na kufikia mafanikio yako

      Asante sana endelea kunifuatilia na utaelimika sana zaidi na zaidi na pia uyafanyie kaz

     Asante sana
          See u next time

Comments

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE