UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA HATUA KWA HATUA
Ufugaji wa kuku wa nyama hatua kwa hatua
Hatua kwa hatua za ufugaji bora wa kuku wa nyama tangu kifaranga hadi kuchinjwa au kuingizwa sokon
Madhumuni ni kukuwezesha wewe mfugaji kupata kuku bora wenye uzito sahihi ,kukuwezesha wewe kupata faida mzuri,Hivyo basi unatakiwa kujua ya kwamba wiki mbili za kwanza za uleaji wa kuku wa nyama unatakiwa kuwa mwangalifu sana
Mambo ya kuzingatia kabla hujaingiza vifaranga wako bandani
Safisha banda la kuku pamoja na mazingira yanayolizunguka yawe safi ikiwa ni pamoja na vyombo vya maji na chakula visafishwe kwa maji safi na salama kwa dawa ili kuuwa vimelea vinavyoweza kusababisha magonjwa
Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga inapaswa kuwa na joto saa moja kabla hujaingiza vifaranga wako bandani
Kwa matokeo chanya hakikisha vifaranga wanafikishwa bandan haraka iwezekanavyo na kama kuna uwezekano wape chakula na maji muda huo huo
Na usisafirishe vifaranga ukiwa umeweka kwenye buti ya gari,mara nyingi wanasafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye siti ya gari ili wapate hewa ya kutosha na kuepuka vifarannga kupata stress au kuchoka
Mambo ya kuzingatia baada ya vifanga kufika bandan
Baada ya kufika tuu bandani unatakiwa uwaondoe vifaranga kwenye box mara moja ,Unapowachelewesha kwenye box hupelekea vifaranga kupata stress na hatimaye hufa au kutokukuwa vizuri
Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa saa 23,ili kuwafanya vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuweza kula chakula vizur bandani
Wape chakula na maji mara tuu uwawekapo bandani ,hakikisha unaongeza vitamin au gucose kwenye maji kabla hujawapa vifaranga wako
Hakikisha unaweka vyombo vya chakula na maji vya kutosha kulingana na kuku ulionao ili kuwawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila shida yoyote
Joto
Banda lako linatakiwa kuwa na joto la kutosha na unaweza kupima joto kwa thermometer
Joto sahihi kwa vifaranga linatakiwa liwe kati ya 40-41 degree centigrade,unaweza pia kupima joto la kuku kwa kuchukuwa mguu wa kuku na kuuweka shavuni na shingoni mwako ukisikia mguu una joto ujue kuku wana joto la kutosha na ukisikia mguu una baridi ujue kuku wanahitaji kuongezewa joto
Joto ni muhimu sana kwa uleaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza hivyo ni vyema kulifatilia kila siku ili kuepuka vifo visivyotarajiwa
Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35
Maji
Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni kiashiria tosha kwamba maji yanavuja,kuna tatizo kwenye chakula au ugonjwa
Kuku kutokunywa maji vizur ni kiashiria tosha kuwa kuku wako wana shida
Kwa kawaida inatakiwa drunker 4 kwa kuku 100 na maji yawe safi na salama na yanakuwepo kwa bandan kwa muda wote wa saa 24 na ieleweke kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa
Chakula
Chakula kinatakiwa kiwekwe kwenye vyombo safi na salama na ambovyo vifaranga vinaweza kula bila shida yoyote kwa siku saba za mwanzo,baada ya hapo anza kuweka chakula kwenye feeders
Kwa feeders za kawaida inashauriwa kuweka feeders 3 kwa kuku 100 na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama na mbali na mwanga,panya na majimaji,epuka kuwapa kuku chakula chenye unyevunyevu na fangasi wa chakula
Aina ya chakula kwa vifaranga
Chick stuster
Wape 0.kg kwa kifaranga kimoja kwa muda wa wiki mbili 2
Grower
Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kwa wiki 2 ,na hii itakuwa ni wiki ya pili tangu umeleta vifaranga wako
Finisher
Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza
Broiler tips
Siku 1-5
Wape glucose na mchanganyiko mmojawapo kati ya hii ifuatayo
Neoxyvital au ctc plus typhorium au trimazin
Fluban na vitamin kama vile broiler boost aminovit au supervit au vitalyte
Kwenye chakula
Weka vigrostat ambayo ina ridocox kwenye chakula,kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya 1-4 ili kuzuia cocidiossis na wiki moja kabla ya kuwauza kwa nyama
Siku ya 6 vitamin Critastress
Siku ya 7
Wape chanjo ya Newcastle masaa mawili baada ya hapo endelea na maji ya vitamin (vitastress)
Wiki ya pili
Chanjo ya Gumboro masaa mawili halafu endelea na maji ya vitamin
Wiki ya tatu
Wape doxycol au 20 % au fluban na ambrolium ,au vitalyte ,molases kwa siku 5-7
Wiki ya nne
Hakikisha kuku wanakuwa kwenye dozi kubwa ya vitamin (vitastress)/vitalyte /broiler boost/supervit broiler
Siku ya tano
Hakikisha kuku wanakuwa kwenye dozi ndogo ya vitamin
Wiki ya sita
Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na maji matupu jion
Baada ya hapo kuku wako watakuwa tayari kwa kuchinjwa au kuingizwa sokoni kwa mauzo
Ukizingatia hayo hakika utapata matokeo mazuri kwenye ufugaji wako au kama ukiona kuna tatizo zaidi mwone daktari wa mifugo kwa ushaur zaidi
Nakutakia ufugaji mwema wenye mafanikio
Kwa elimu zaidi bofya link
https://chat.whatsapp.com/7BXGRSO9DwYFoEaiESaoFq
Kuingia darasan
Au wasiliana na mm kwa namba
+255753637565
Sofia Mutashobya
By kwa sasa
Comments
Post a Comment