USIKATE TAMAA KWASABABU YA CHANGAMOTO UNAZOPITIA

CHANGAMOTO UNAZOPITIA ZISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUKATA TAMAA NA KUSHINDWA KUSONGA MBELE 

Mara nyingi binadamu hughairi kufanya mambo hata yale yanayohusu ustawi wake kwa kuhofia  ama kukosea au kushindwa kabisa,yaani kutoweza. Wakati mwingine huahirisha kuendelea Mara baada ya kukutana na vikwazo vya kufeli ama kupata hasara katika biashara au jambo fulani alilokuwa akilitegemea katika maisha yake

Ukweli ni kwamba kila mpambanaji katika maisha haya hufeli na kukosea kabla hajafanikiwa . Na unapokosea ndo unajifunza na ufanye uchunguzi ni wapi ulipokosea ili ujirekebishe ,usiishi na maumivu ya vitu vilivyokukwamisha mwanzo,futa ,sahau fungua ukurasa mpya wa kusaka mafanikio yako

Jambo la kujiuliza hapa ni Wewe unapofanya jambo lako na ukabaini kuwa ama halijakubalika au limefeli huwa unafanya nini?. Je, unaendelea au unakata tamaa na kuachana nalo?

Ni muhimu sana kuchukulia kufeli kwako kama sehemu ya kujifunza . Kufeli ni nafasi nzuri ya kuanza upya tena kwa namna bora zaidi kuliko awali. Usiruhusu kukata tamaa kirahisirahisi. Wewe ni Mshindi.

Je, umeanzisha biashara na imefeli?, Pengine  Umeanzisha mradi na umeambulia hasara kubwa na aibu? au Hata umefanya mtihani na umefeli vibaya?. Umeamua nini baada ya haya yote? USIKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI

Nataka kuzungumza na wewe nikikutia moyo kwamba, Changamoto hii unayoipitia sio kikwazo, jambo la msingi chukuwa maamuzi sahihi yatakayokusha kutoka eneo moja kwenda jingine kwa nguvu na uwezo ulionao Epuka kuishi na maumivu
   
Tuko pamoja see you soon

Comments

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE