JINSI YA KUDARIZI

JIFUNZE JINSI YA KUDARIZ
Je ungependa kujifunza jinsi ya kudarizi vitambaa vya makochi,mashuka,foronya za kitandani pamoja na kwenye makochi nifuatilie katika masomo yangu hatua kwa hatua  ili uweze kujifunza

Lakini tutaanza na kujifunza jinsi ya kudarizi vitambaa
          MAHITAJI

1)Mashine ya kudarizi
2)Kitambaa
3)Nyuzi za rangi
4)Binding/au urembo wa less
5)Tape measure ya kupimia kitambaa
6)Karatasi iliyochorwa mauwa
7) Cabornpaper
8)Ringi ya kubana kitambaa wakati wa kudariz

Hayo ndio mahitaji muhimu yanayotakiwa unataka kudariz kitambaa na kama yanavyoonekana hapo juu kwenye picha

      Jinsi ya kudarizi hatua kwa hatua

1)Andaa kitambaa ,kitambaa kinatakiwa kiwe cha tetron ndio kifaa zaidi kwa kudarizi ,kisha pima kulingana na zaiz ya kitambaa unachotaka ,aidha ni kidogo au kikubwa ,kwa kawaida kikubwa kinakuwa ni mita moja ambayo ni cm 100 urefu na upana ulingane  au utakavyopenda mwenyewe,na kidogo  cm 16 kwa 16 urefu na upana ulingane ila ukitaka kikubwa zaidi unaweza ukaongeza ,au kama ni kidogo ukapunguza

2)Ukishamaliza kupima kitambaa chako chukua caborn paper weka juu ya kitambaa ,kisha chukuwa karatasi uliyochora mauwa na uweke juu ya kabon paper na uanze kuchora mauwa kwa kutumia kalamu hadi uwa liishe lote,kisha ondoa kabonpaper na karatasi na utaona mauwa yametokea kwenye kitambaa

3)Chukuwa kitambaa chako na ukibane kwa kutumia ringi,hakikisha kitambaa chako kimekaza vizur ili kisikusumbuwe wakati wa kudarizi

4)Baada ya hapo andaa mashine pamoja na nyuzi  za kudarizia,kisha tunga uzi kwenye mashine ,kisha chukuwa kitambaa chako na uanze kudarizi  hadi ua lote liishe

5)Ukishamaliza kudariz ,chukua binding na uishonee kwenye kitambaa hadi kiishe na baada ya hapo kitambaa chako kitakuwa tayar kwa matumizi yako mwenyewe au kwa kuuzwa

Hiyo ndio jinsi ya kudarizi vitambaa ,kwa leo naishia hapa
  Usiache kunifuatilia sehemu ya pili ya mfulizo wa masomo haya na tutajifunza jinsi kushona foronya  pamoja mashuka

Kama umependa mafunzo haya  bonyeza link https://chat.whatsapp.com/98Rie34AujmKMTDAnoc0DH

Kuingia darasani,au nitumie ujumbe whatsup kwa namba 0753637565
      Au coment neno nataka
  Nitakuingiza darasani ili uweze kujifunza zaidi na zaidi

     . By Sofia Mutashobya

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE