JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU

      MAHITAJI

1.    Unga wa dengu ½ kilo
2.    Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani
3.    Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
4.    Unga wa mchele ¼ kilo
5.    Chumvi kiasi
6.    Mafuta ya alizeti ½ lita
7.    Baking powder

JINSI YA KUPIKA

1)Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga.

2) Baada ya hapo changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.

3)Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa.

4) Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.

5)Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa au kuuzwa

Na huo ndio upikaji wa tambi za dengu

    Asante sana

Comments

  1. Allah awazidishie kwa kutufundisha hizi mbinu za ujasiriamal!

    ReplyDelete
  2. Inayotumika ni baking powder or baking soda?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE