Posts

Showing posts from February, 2019

JINSI YA KUTENGENEZA KIKOI CHA BATIKI

Image
UTENGENEZAJI WA KIKOI CHA BATIKI       Mahitaji Kitambaa cha batiki Sodium hydrosalfate Caustic Soda Maji Ndoo ya kukorogea rangi Rangi Mkasi Kamba Mask Gloves Jinsi ya kutengeneza 1)Andaa kitambaa cha batiki mita 2 kisha tandika kwenye meza au sakafu 2)Kunja kitambaa kulingana na mauwa unayoyataka na ufunge kwa kamba 3)Baada ya hapo tengeneza rangi kisha chovya kitambaa chako kwenye rangi sehemu ulizokunja na kufunga,kisha kitoe kiache kwa dakika 10-25 4)Fungua kitambaa na ukianike kivulin ,kisha kitoe na ukifue kwa maji barid bila sabuni,halafu anika kivulin mpaka kikauke 5)Baada ya kukauka chukuwa kitambaa,kwenye upana wa kitambaa pemben na pemben chana kidogo kwa mkono na chukuwa sindano na uanze kutoa nyuzi kwa saiz ambayo unataka kikoi chako kiwe,kisha funga nyuzi ulizofumua kisha piga pas kikoi kitakuwa tayar kwa matumiz NB:Unaweza ukafumua nyuzi kwanza ndo ukakunja mauwa ,jinsi utakavyoona inafaa Na kikoi kitakuwa na muonekano kama tunavyoona kwenye pic

LEBO NI NN

LEBO      Lebo ndio wasifu wa bidhaa wapendwa. Lebo pia hubuniwa kwa mwonekano wake ikiwa na mambo yafuatayo: 1: *Jina la bidhaa.* Buni jina zuri lenye mvuto ambalo mteja atavutiwa nalo na kulikumbuka kwa urahisi. Pia unaweza kutumia jina la kampuni, kikundi au jina lako. Mfano *Mary Clips* 2: *Utambulisho.* Andika utambulisho wa bidhaa ili mteja ajue ni bidhaa gani. Kwa mfano *Clips* 3: *Vilivyomo{Ingredients}.* Andika vitu vyote ulivyochanga ili kupata bidhaa hiyo. Mfano *mwarobaini, mafuta ya mawese, caustic soda, chumvi na glycerine.* 4: *Ujazo au uzito{quantity}.* Andika ujazo au uzito wa bidhaa. Mfano *200mil, 25kg, n.k* 5: *Tarehe au ujazo na idadi ya bidhaa ulizotengeneza(batch no) mfano *30-01-2019, 200g, 375* 6: *Tarehe iliyotengenezwa(mf.Date) na tarehe ya mwisho wa matumizi(exp. Date)* Mfano: Mfg.30 Jan,2019               Exp.30 Jan, 2020 N.B: *Bidhaa za sabuni na vipodozi hudumu kwa muda wa miaka mitatu na bidhaa za vyakula hudumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya kuoshea tiles,masinc na vigae

Image
Tiles  cliner  ni  dawa  ya  kusafisha  marumaru,  masinki  ya  choo  na  ya kunawia.  *Hutengenezwa  kwa  kutumia  malighafi  zifuatazo.* 1; Maji  lita 20 2: Hydrokloliki  aside  15lt  3: Siles 500gm *JINSI YA  KUTENGENEZA* 1. Pima  maji  20lts  weka  kwenye  diaba 2. Weka  siles  500gm  anza kukoroga  kuelekea  upande  mmoja 3. Weka  Hydrokololic  aside  polepole  koroga  baada  ya  hapo  itakuwa tayari  weka  kwenye  vifungashio. Itakuwa tayari kwa matumizi au kuuzwa Asante

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

Image
🍦🍦1.ICE CREAM ZA UBUYU🍦🍦 🍦mahitaji:-   ubuyu wa unga 1/2   sukari 3/4   ngano vijiko vi 2.    Rangi yoyote   maji litre8-10   vannila/hiliki. 🍦🍦Weka maji, weka ubuyu wa unga nusu kilo.  ubuyu changanya kbs na unga wa ngano vijiko viwili. 🍦🍦bandika jikoni huku ukikoroga mpaka uwe mzito kiasi. weka sukari pia chota hata sehemu tatu ili kuweka rangi tofauti. koroga dk 5 then epua pooza na ufunge kwenye vifuko. N:B Unga wa ngano unafanya ice cream iwe laini isiwe ngumu. badala ya ngano unaweza weka corn flour. japo ni gharama kdg Hivyo ndivyo unaweza kutengeneza ice cream ya ubuyu hatua kwa hatua Asante na usiache kutembelea blog hii Pia nifuatilie kwenye ukurasa wangu wa Facebook Na Page yangu kwa jina la Sofia Mutashobya Anza Hata Kama Haupo Tayari Simu 0753637565