LEBO NI NN

LEBO

     Lebo ndio wasifu wa bidhaa wapendwa. Lebo pia hubuniwa kwa mwonekano wake ikiwa na mambo yafuatayo:

1: *Jina la bidhaa.* Buni jina zuri lenye mvuto ambalo mteja atavutiwa nalo na kulikumbuka kwa urahisi. Pia unaweza kutumia jina la kampuni, kikundi au jina lako. Mfano *Mary Clips*

2: *Utambulisho.* Andika utambulisho wa bidhaa ili mteja ajue ni bidhaa gani. Kwa mfano *Clips*

3: *Vilivyomo{Ingredients}.* Andika vitu vyote ulivyochanga ili kupata bidhaa hiyo. Mfano *mwarobaini, mafuta ya mawese, caustic soda, chumvi na glycerine.*

4: *Ujazo au uzito{quantity}.* Andika ujazo au uzito wa bidhaa. Mfano *200mil, 25kg, n.k*

5: *Tarehe au ujazo na idadi ya bidhaa ulizotengeneza(batch no) mfano *30-01-2019, 200g, 375*

6: *Tarehe iliyotengenezwa(mf.Date) na tarehe ya mwisho wa matumizi(exp. Date)*
Mfano: Mfg.30 Jan,2019
              Exp.30 Jan, 2020

N.B: *Bidhaa za sabuni na vipodozi hudumu kwa muda wa miaka mitatu na bidhaa za vyakula hudumu kwa muda wa mwaka mmoja.*

Zipo *lebo* za aina mbili. Ya kwanza ni ile ya muhuri ambayo hugongwa kwenye bidhaa yenyewe na ya pili ni ile inayowekwa kwenye kifungashio ambayo ni ya karatasi yenye kung'ara(stika)

Kwa hiyo hakikisha unaweka bidhaa yako lebo ili kuiongozea ubora zaid

Asante endelea kutembelea blog hii

Comments

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE