JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA NAZI

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA NAZI KWA NJIA RAHISI UKIWA  NYUMBANI KWAKO


Mafuta  ya  nazi Ni  bidhaa  ambayo  hutokana  na  nazi  hufanya  kazi  nyingi  sana  mwilini ikiwemo kuondo  makovu  na  mabaka  na  kuacha  mwili  ukiwa  laini  na  bila  mafuta  na hutumika sana mara  nyingi  katika kutengenezea sabuni  za  vipande.

MAHITAJI

1: Sufuria hutumika kwa ajili  ya kupikia mafuta yako  jikoni.

2: Blenda  au  kibao cha  mbuzi  kwa  ajili  ya  kukunia  nazi  zako  ili  uweze  kupata tuwi la nazi.

3: Chujio  kwa  ajili  ya  kuchuja  machicha  ya  nazi  na  kuweza  kupata  tuwi  likiwa safi  kabisa.

4: Jiko  lenye  moto  hili  hutumika  kwa  ajili  ya  kuchemsha  mafuta  yetu  ili yajitenge  na maji.

5. Friji  kama lipo  kwa ajili  ya kugandishia .

MALIGHAFI

 1: Nazi  safi  na nzima.

2: Maji 


Jinsi ya kutengeneza


1. Kwanza andaa nazi zako zikiwa safi.

2. kisha kuna nazi zako zote  kwa kutumia kibao cha mbuzi au kama una blenda unaweza ukatumia kupata nazi iliyokunwa. 

3. Ukishapata nazi iliyokunwa unatakiwa kuichuja kwa kutumia *chujio* ili kupata *tuwi* la nazi  na unaweza ukaongeza maji kidogo ili kupatatuwi jingi kidogo na hilo  tuwi ndio ambalo tunalolihitaji kwa ajili ya kuitumia. 

4. Kisha utailaza *tuwi* lako mpaka kesho ili kutenganisha maji na tuwi na mafuta , hapo litatengeneza tabaka na kisha utatoboa hilo tabaka ili kutoa maji yote ndani ya tuwi lako. 

5. kisha bandika *jikoni* ilo tuwi lililo ganda ili kupata mafuta halisi.

6. Kisha baada ya kubandikwa katika moto yatabadilika na kuwa mafuta safi kabisa bila tatizo lolote. 



BAADHI YA FAIDA ZINAZO TOKANA NA MAFUTA YA NAZI

 1. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu.

2. Huzuia uwezekano wa kupata kansa.

3. Yanaongeza kinga ya mwili mara dufu.

4. Yanaongeza nguvu za ubongo

5. Yana ongeza nguvu za uvumilivu.

6. Dawa nzuri kwa matatizo ya mifupa.

Hizo ndizo faida zitokanazo na mafuta haya ya nazi

Kwa elimu zaidi niandikie ujumbe whatsup kwa namba

0753637565/0714763386
Au
Nipigie kwa hizo namba hapo

Asante

Comments

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE