JINSI YA KUPIKA KEKI

UPIKAJI WA KEKI
JIFUNZE KUPIKA KEKI KWA JIKO LA MKAA.

Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake.
MAHITAJI
- unga vikombe2
-Maziwa kikombe1
-Sukari kikombe1
-Siagi kikombe1
-Baking powder vijiko vidogo 2
-Mayai 6 yakienyeji
-Vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao. Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda.

HATUA ZA UPIKAJI

-Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako

-Chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari.

-Koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa
-Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mchanganyiko wako bila kupumzisha mkono

-Weka matone mawili ya vanilla au maganda ya limao huku ukiendelea kuchanganya.

-Weka unga vikombe viwili uliochanganywa na baking powder kwenye mchanganyiko wako na endelea kuukoroga taratibu

-Baada yahapo tia maziwa kikombe kimoja nauchanganye taratibu

-Mimina taratibu mchanganyiko wako kwenye sufuria maalumu yakupikia iliyopakwa siagi. Zingatia Iwapo utapenda keki yako iwe na rangi unaweza ukaweka kokoa kwenye mchanganyiko wako.
-Weka sufuria ya mchanganyiko katika jiko lenye joto la wastani kwa muda wa nusu saa

-Baada ya hapo toa keki yako tayari kwakuliwa


Kwa mafunzo zaidi wasiliana nasi kwa namba

0753637565/0714793386

Au tuma ujumbe whatsup kwa hizo namba utapewa maelekezo

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

JINSI YA KUANDAA UNGA WA LISHE