Posts

Showing posts from September, 2018

JIFUNZE NIDHAMU YA PESA

Image
MAMBO MATANO YATAKAYOKUSAIDIA KUWA NA NIDHAMU JUU YA PESA    Fuatana nami twende tukajifunze maana hili eneo ni changamoto kwa walio wengi  wetu na ndipo makosa makubwa yanapofanyika na tunaishia kulalamika tyuu           Mambo muhimu na ya msingi kabisa 1)Kubali tatizo ulilonalo kuwa ni lako mwenyenyewe,kiri tatizizo la kutokuwa na matumizi sahihi ya mara tuu upatapo pesa  ,halafu tafuta suluhisho la tatizo lako ufanye nini cha kukuwezesha kuachana na matumizi mabovu ya pesa 2)Jifunze kuweka malengo ya maisha au kile ambacho unakifanya kifanikiwe na uwe na nidhamu nacho na kikifanya kiwe cha kwanza kwako kuliko mambo mengine na ukipata pesa peleka kwenye malengo makubwa kwanza,mfano umejiwekea malengo baada miez mitano unataka ujenge nyumba,au nifungue biashara  nk hakikisha unapopata pesa ipeleke kwenye ujenz,au biashara uliyokusudia kwanza   3)Kuwa na mpango mkakati( plani)Hata kama hauna pesa kwa muda huo jiweke mkakati au mbinu bora kwa kuweka akiba ya pesa ili uweze k

USIKATE TAMAA KWASABABU YA CHANGAMOTO UNAZOPITIA

CHANGAMOTO UNAZOPITIA ZISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUKATA TAMAA NA KUSHINDWA KUSONGA MBELE  Mara nyingi binadamu hughairi kufanya mambo hata yale yanayohusu ustawi wake kwa kuhofia  ama kukosea au kushindwa kabisa,yaani kutoweza. Wakati mwingine huahirisha kuendelea Mara baada ya kukutana na vikwazo vya kufeli ama kupata hasara katika biashara au jambo fulani alilokuwa akilitegemea katika maisha yake Ukweli ni kwamba kila mpambanaji katika maisha haya hufeli na kukosea kabla hajafanikiwa . Na unapokosea ndo unajifunza na ufanye uchunguzi ni wapi ulipokosea ili ujirekebishe ,usiishi na maumivu ya vitu vilivyokukwamisha mwanzo,futa ,sahau fungua ukurasa mpya wa kusaka mafanikio yako Jambo la kujiuliza hapa ni Wewe unapofanya jambo lako na ukabaini kuwa ama halijakubalika au limefeli huwa unafanya nini?. Je, unaendelea au unakata tamaa na kuachana nalo? Ni muhimu sana kuchukulia kufeli kwako kama sehemu ya kujifunza . Kufeli ni nafasi nzuri ya kuanza upya tena kwa namna bora zaidi kuli

JUA JINSI YA KUKUZA JINA LAKO (BRAND YAKO)

Image
JUA NI JINSI GAN UNAWEZA KUJENGA AU KUKUZA JINA LAKO (Brand) AIDHA NI JINA LA BIASHARA ,COMPANY AU JINA LAKO BINAFSI Kwanza kabisa sifa ya kwanza ni upekee wa jina lako ,jina lako lina dhamani kubwa sana  (personal style) wewe ni nani na ukisimama uonekane wewe kama wewe usifananishwe na mtu mwingine kuanzia muonekano,kuongea hata mambo unayoyafanya 2)Ongeza network ungana na watu wanaofanya kitu kinachofanana na chako jifunze zaidi na zaidi kutoka kwao,kama ww ni mfugaji ungana na wafugaji,mfanyabiashara ungana nao,sio wewe ni mkulima unakaa na waimbaji hiyo haitakusaidia kaa kwenye nafasi 3)Zungumza kile kitu unachokifanya kila wakati kiishi au kukitangaza lile jambo unalofanya leo hii tunaona makampuni makubwa,watu maarufu wenye majina makubwa ni kwasababu ya kuzungunguza na kutangaza wanachokifanya usiwe na kitu ukabaki nacho mwenyewe (share) na wengine hata kwenye mitandao ya kijamii elezea kitu unachokifanya na watu watakuelewa sana 4)Kitu kingine cha msingi sana ni kuj

ULEAJI WA VIFARANGA KWA NJIA YA ASILI

Image
KULEA VIFARANGA KWA NJIA YA ASILI: Kuku aliyetotoa vifaranga anaweza kuachiwa avilee, lakini ili kuepuka majanga kama vile vicheche na mwewe inashauriwa watunzwe ndani ya uzio utakaowazuia ndege hao hatari kuingia na kuwachukua. Kulea vifaranga kwa kutumia tetea ni njia ya asili itumikayo kuatamia, kuangua, kutotoa na hatimaye kuvilea hadi hapo wanapoanza kujitafutia chakula na kujihami dhidi ya maadui.  Ili kutumia njia hii katika kuangua mayai kukutolesha mayai na kulea vifaranga ni lazima upate kuku mwenye tabia ya kuatamia (broody hen). Kiota cha kuku anayeatamia hutengwa kutoka kwenye viota vya kutagia. Viota hivi huwekwa matundu mawili ya kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Ukubwa wa matundu hayo ni inchi mbili za upana na urefu. Andaa marandio mapya na kuweka mayai ya kuangua juu yake; chukua mayai ya kutosha kwenye kiota lakini yasizidi yale anayoweza kulalia  au kuyaatamia (kiasi cha mayai kumi na moja yanatosha kwa tetea mmoja). Weka kiota sehemu isiyo na usumbufu

RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA HATUA KWA HATUA

Image
RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA Kuku chotara/kienyeji hufungwa kwa matumizi ya kutaga mayai na pia kwa nyama.Mfugaji atachagua aina na mfumo wa chakula kutokana na yeye anafuga kuku hawa kwa matumizi gani. Ili kuku wafugwe kwaajili ya mayai fuata ratiba hii ya chakula Chick starter kwa muda wa miezi miwili(2) Grower Mash kwa muda wa miezi miwili na nusu(2.5) Layers mwezi mmoja na kuendelea. Ili kuku wafugwe kwaajili ya nyama fuata ratiba hii ya chakula Broiler starter-mwezi mmoja(1) Grower Mash-Mwezi mmoja(1) Broiler Finisher-Mwezi mmoja(1) Ili kuku wafugwe na kutaga mayai kwaajili kutotolesha fuata ratiba hii ya chakula Chick Starter-miezi miwili(2) Grower mash-miezi miwili na nusu(2.5) Breeders mash-mwezi mmoja na kuendelea.hakikisha majogoo wanapunguzwa na kubaki na uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea kumi(1:10) Ratiba hii ni kwa ufugaji wa kibiashara lakin mfugaji anaweza kuwafuga kuku hawa kwa mfumo wa nusu huria yaani kuku akaachiwa ajitaft

FUATA KANUNI ZA UFUGAJI BORA KIBIASHARA

Image
KANUNI ZA UFUGAJI BORA LISHE BORA ENDELEVU KWA MATOKEO BORA ZAIDI Mfugaji ili uwape kuku wako lishe bora yenye kuendelea, na ili upate matokeo bora zaidi katika ufugaji wako wa kuku basi yakupasa kuzingatia yafuatayo:- Tumia chakula bora na siyo bora chakula. Tumia chakula bora ambacho hakina madhara kwa kuku wako na hata walaji kwa ujumla. Weka chakula mahali safi na salama kuepuka wadudu waharibifu kama vile panya ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kwa kuku. Tumia kanuni ya "least cost combination" yaan tumia chakula cha bei nafuu kinachotoa matokeo bora zaidi ili kupunguza gharama za ufugaji hali ambayo itakufanya upate faida mara dufu. Kwa kufanya hivyo utaweza kuwalisha kuku wako chakula kilicho bora kwa matokeo bora zaidi bila kuyumba kiuchumi wakati wote wa ufugaji wako. KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI Kuna usemi usemao "mali bila daftari hupotea bila habari" ukiwa na mradi wowote wa ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu za kila siku au kwa kila

UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA HATUA KWA HATUA

Image

ILI UWEZE KUFANIKIWA IJUE SIRI HII

MOJA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA LAZIMA UJIFUNZE KUWA MVUMILIVU   Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara inakupasa kuwa na uvumilivu huwezi anza biashara leo na ufanikiwa leo leo itachukuwa muda na inategemea na aina ya biashara unayofanya       Hapa nakueleza kitu cha msingi sana na kitakusaidia sana katika kufanya biashara yako Lazima ukubali kuwa mvumilivu. Inawezekana ikatokea mapema Zaidi ya miaka mitano kutokana na aina ya kile unachokifanya. Pia inawezekana ukapata nguvu kubwa kutoka kwa watu ambao watakuja kukusaidia ukavuka haraka lakini mimi sikufundishi juu ya vitu ambavyo havitokani na nguvu yako mwenyewe. Ni kweli unaweza kufanikiwa kufikia hao elfu moja mapema Zaidi kulingana na watu ambao ulionao wewe. Na inaweza kuchukua hata miaka 5 hadi kumi kwa mtu kuweza kufikia kwenye elfu moja. Unajua watu elfu moja wanaweza kukupa kitu gani? Tusema hao watu elfu moja wanaweza kununua bidhaa kwako ambazo kwa jumla ndani ya mwezi mmoja utaweza kutengeneza tsh elfu kumi tu kwa k