Posts

JINSI YA KUTENGENEZA KIKOI CHA BATIKI

Image
UTENGENEZAJI WA KIKOI CHA BATIKI       Mahitaji Kitambaa cha batiki Sodium hydrosalfate Caustic Soda Maji Ndoo ya kukorogea rangi Rangi Mkasi Kamba Mask Gloves Jinsi ya kutengeneza 1)Andaa kitambaa cha batiki mita 2 kisha tandika kwenye meza au sakafu 2)Kunja kitambaa kulingana na mauwa unayoyataka na ufunge kwa kamba 3)Baada ya hapo tengeneza rangi kisha chovya kitambaa chako kwenye rangi sehemu ulizokunja na kufunga,kisha kitoe kiache kwa dakika 10-25 4)Fungua kitambaa na ukianike kivulin ,kisha kitoe na ukifue kwa maji barid bila sabuni,halafu anika kivulin mpaka kikauke 5)Baada ya kukauka chukuwa kitambaa,kwenye upana wa kitambaa pemben na pemben chana kidogo kwa mkono na chukuwa sindano na uanze kutoa nyuzi kwa saiz ambayo unataka kikoi chako kiwe,kisha funga nyuzi ulizofumua kisha piga pas kikoi kitakuwa tayar kwa matumiz NB:Unaweza ukafumua nyuzi kwanza ndo ukakunja mauwa ,jinsi utakavyoona inafaa Na kikoi kitakuwa na muonekano kama tunavyo...

LEBO NI NN

LEBO      Lebo ndio wasifu wa bidhaa wapendwa. Lebo pia hubuniwa kwa mwonekano wake ikiwa na mambo yafuatayo: 1: *Jina la bidhaa.* Buni jina zuri lenye mvuto ambalo mteja atavutiwa nalo na kulikumbuka kwa urahisi. Pia unaweza kutumia jina la kampuni, kikundi au jina lako. Mfano *Mary Clips* 2: *Utambulisho.* Andika utambulisho wa bidhaa ili mteja ajue ni bidhaa gani. Kwa mfano *Clips* 3: *Vilivyomo{Ingredients}.* Andika vitu vyote ulivyochanga ili kupata bidhaa hiyo. Mfano *mwarobaini, mafuta ya mawese, caustic soda, chumvi na glycerine.* 4: *Ujazo au uzito{quantity}.* Andika ujazo au uzito wa bidhaa. Mfano *200mil, 25kg, n.k* 5: *Tarehe au ujazo na idadi ya bidhaa ulizotengeneza(batch no) mfano *30-01-2019, 200g, 375* 6: *Tarehe iliyotengenezwa(mf.Date) na tarehe ya mwisho wa matumizi(exp. Date)* Mfano: Mfg.30 Jan,2019               Exp.30 Jan, 2020 N.B: *Bidhaa za sabuni na vipodozi hudumu kwa muda wa miaka mitatu na ...

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya kuoshea tiles,masinc na vigae

Image
Tiles  cliner  ni  dawa  ya  kusafisha  marumaru,  masinki  ya  choo  na  ya kunawia.  *Hutengenezwa  kwa  kutumia  malighafi  zifuatazo.* 1; Maji  lita 20 2: Hydrokloliki  aside  15lt  3: Siles 500gm *JINSI YA  KUTENGENEZA* 1. Pima  maji  20lts  weka  kwenye  diaba 2. Weka  siles  500gm  anza kukoroga  kuelekea  upande  mmoja 3. Weka  Hydrokololic  aside  polepole  koroga  baada  ya  hapo  itakuwa tayari  weka  kwenye  vifungashio. Itakuwa tayari kwa matumizi au kuuzwa Asante

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

Image
🍦🍦1.ICE CREAM ZA UBUYU🍦🍦 🍦mahitaji:-   ubuyu wa unga 1/2   sukari 3/4   ngano vijiko vi 2.    Rangi yoyote   maji litre8-10   vannila/hiliki. 🍦🍦Weka maji, weka ubuyu wa unga nusu kilo.  ubuyu changanya kbs na unga wa ngano vijiko viwili. 🍦🍦bandika jikoni huku ukikoroga mpaka uwe mzito kiasi. weka sukari pia chota hata sehemu tatu ili kuweka rangi tofauti. koroga dk 5 then epua pooza na ufunge kwenye vifuko. N:B Unga wa ngano unafanya ice cream iwe laini isiwe ngumu. badala ya ngano unaweza weka corn flour. japo ni gharama kdg Hivyo ndivyo unaweza kutengeneza ice cream ya ubuyu hatua kwa hatua Asante na usiache kutembelea blog hii Pia nifuatilie kwenye ukurasa wangu wa Facebook Na Page yangu kwa jina la Sofia Mutashobya Anza Hata Kama Haupo Tayari Simu 0753637565

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI

Image
Mahitaji Caustic Soda kilo 3 Mafuta ya mawese lita 20 Sodium Silket Maji lita 10 Rangi ya bluu vijiko 3 Jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua 1)Chukuwa coustic soda changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizur baada ya hapo iache kwa saa 24 2)Chukuwa kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni,weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizur kabisa 3)Chukuwa coustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa ,kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka,tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja 4)Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo ,chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kias kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizur 5)Kishaa andaa box la kukaushia sabuni na mimina mkorogo wa...
Image
Hay   Jina langu naitwa Sofia Mutashobya ,     Ninawasaidia wajasiriamali watarajiwa jinsi ya kuanzisha viwanda majumbani mwao vyenye kutengeneza bidhaa mbali mbali kama hizi zifuatazo:  Sabuni za mche,sabuni ya unga,sabuni za kuoshea tiles,masinc ya choo,losheni,shampoo,sabuni za magadi ,sabuni za usafi za maji,kufulia ,kunawia mikono ,tishet na aina zote za batiki .Pamoja na mbinu za ufugaji bora wa kuku kisasa na kibiashara ,chanjo za magonjwa ya kuku na ratiba zake ili kuweza kuweza kujiajiri wenyewe na kujitengenezea kipato      Kama unapenda kupata mafunzo haya coment hapa chini neno UJASIRIAMALI  nkutumie link ya kujiunga na mafunzo haya Mafunzo ni bure kabisa          Karibu sana

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU       MAHITAJI 1.    Unga wa dengu ½ kilo 2.    Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani 3.    Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai 4.    Unga wa mchele ¼ kilo 5.    Chumvi kiasi 6.    Mafuta ya alizeti ½ lita 7.    Baking powder JINSI YA KUPIKA 1)Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. 2) Baada ya hapo changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja. 3)Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. 4) Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo...